Leicester City wamemuuza Luis Hernandez kwa klabu ya Malaga
kwa ada isiyojulikana, miezi sita baada ya kumsaini difenda huyo.
Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 27, alishiriki mechi
nane baada ya kujiunga na mabingwa hao wa Ligi ya Premia kutoka Sporting Gijon
mwezi Julai
Amesaini mkataba wa miaka mitatu na nusu na klabu ya Malaga,
ambao wamo katika nafasi ya 14 katika ligi ya Uhispania.
Mechi yake ya mwisho kuwachezea Leicester ni walipokabiliana
na Bournemouth tarehe 13 mwezi Disemba mwaka jana walipopata ushindi wa 1-0.
Chanzo: Sport News
No comments:
Post a Comment