Michezo miwili ya mwisho ya hatua ya makundi ya michuano ya
Afcon 2017 imemalizika kwa Misri kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ghana
na hivyo kuongoza kundi D kwa alama 7 huku Ghana wakiwa nafasi ya pili kwa
alama 6.
Bao la ushindi la mafarao wa Misri lilifugwa na nyota wao
Mohamed Salah, katika dakika ya 11 ya mchezo kwa mkwaju mkali wa mpira wa
kutenga uliokwenda moja kwa moja nyavuni.
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo timu ya Uganda
walitoshana nguvu na Mali kwa kufungana bao 1-1.
Michezo ya hatua ya robo fainali itaanza kuchezwa jumamosi
ya terehe 28 kwa Burkina Faso kucheza na Tunisia huku Senega wakicheza na
Cameroon.
Jumapili kutacheza michezo miwili ya robo fainali ya pili
kwa DR Congo kuchuana na Ghana nao Misri wakipimana ubavu na Morroco.
No comments:
Post a Comment