Programu za simu za kisasa aina ya 'Smart Phone' kila siku
zinaendelea kutumika katika nyanja mbali mbali za maisha na shughuli za kila
siku za mwanadamu.
Nchini Sudan Kusini mara kwa mara imetambulishwa kwa kuwa
eneo la vita ,mauaji na ghasia,sasa matumaini yameanza kupnekana baada ya raia
wa kawaida katika nchi hiyo kuanzisha programu ya michezo ya simu inayosisitiza
amani na umoja baina ya wananchi.
Luan Michael Mayen ni kijana mwenye umri wa miaka 24
aliyeunda programu hiyo mpya ya simu inayotambulika kwa jina la 'Salaam'.
Programu hiyo ambayo ni mchezo wa simu unachezwa na mchezaji
kwa kuharibu mabomu yote yaliyotegwa,kabla hayajalipuwa raia wasio na hatia,ikiwa
mchezaji ameweza kuharibu mabomu yote,ujumbe wa hongera kwa kuokoa maisha ya
watu unatumwa .
Kampuni ya Mayen ina programu maalum ya michezo kwa jina la
'Junub'.
Katika michezo hiyo kuna majina kama 'Wahda' inayomaanisha
umoja huku Salaam inamaanisha amani.
Mayen ana lengo la kusambaza michezo hiyo kwa raia 200,000
walioko katika kambi za wakimbizi Uganda baada ya kutoroka wakati wa ghasia
nchini Sudan Kusini.
No comments:
Post a Comment