Baada ya kupotea kwa muda mrefu katika ulingo wa masumbwi,
bingwa wa zamani wa dunia wa I.B.O Mbwana Matumla amesema bado hajastaafu ngumi
na kuwataka mashabiki wake waje kuona ufundi mpya aliokuja nao wakati
atakapomvaa Shaban Selemani katika pambano la raundi sita litakalochezwa
Februari tano katika uwanja wa ndani wa taifa jijini Dar es Salaam.
Mkali huyo anayetokea katika familia ya masumbwi na kuwahi
kutamba ndani na nje ya nchi na kuwahi kutwaa mikanda ya ubingwa wa WBA,IBO,ICB
na Asian Pacific amesema hajafikiria kustaafu kucheza ngumi kwa kuwa bado ana
uwezo kuendelea kupambana ulingoni hivyo amewataka mashabiki wake kufika kwa
wingi siku hiyo kujionea ufundi mpya alioibuka nao kutoka mafichoni.
Mbwana atacheza pambano hilo lisilo la ubingwa likiwa ni la
utangulizi huku pambano kubwa litakuwa ni kati ya Ramadhani Shauri dhidi ya
Meshack Mwankemwa la kuunganisha mikanda ya taifa wa TPBC na wa Afrika
Mashariki na kati ambapo leo matumla amepata fursa ya kucheza Sparing dhidi ya
bondia Mwankemwa.
No comments:
Post a Comment