Uamuzi wa Donald Trump kupiga marufuku wahamiaji wa kiislamu
kutoka kwenye nchi zenye raia wengi wa dini hiyo, umesababisha hasira kuu
duniani kote na wahamiaji wakikataliwa kupanda ndege kuingia Marekani.
Raia waliokuwa na hati za kusafiria kutoka Iran, Iraq,
Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen walizuiliwa kwenye viwanja vya ndege,
wakati wale waliokuwa wameshapanda ndege walishikiliwa baada ya kutua Marekani.
Katika tukio moja, abiria watano wa Iraq na mmoja wa Yemeni,
waliokuwa na visa halali, walizuiliwa kupanda ndege ya EgyptAir iliyokuwa
ikitoka Cairo kwenda New York na hatimaye kuelekezwa kwenye ndege zinazorudi
kwenye nchi zao.
Mwanamke mmoja aliyekiambia mauaji ya Isis nchini Iraq mwaka
2014, alizuiliwa kupanda ndege mjini Baghdad, baada ya kusubiria visa kwa miezi
mingi ili akaungane na mumewe ambaye tayari yupo Marekani. Rais Trump amepiga
marufuku kwa miezi mitatu wakimbizi toka nchi saba duniani, ili kuchuja magaidi
wa kiislamu wasiingie nchini humo.
Wakimbizi kutoka Syria wamepigwa marufuku kimoja.
Hata hivyo, jaji mmoja alitoa ruhusa Jumamosi kwa raia
kutoka nchi hizio saba waliokuwa wameshaingia nchini humo, wale waliokuwa
njiani, wenye visa halali kukaa Marekani. Waandamaji kadhaa walikusanyika
kwenye viwanja vya ndege nchini Marekani Jumamosi hii kupinga uamuzi huo wa
Trump. Maandamano zaidi yatafanyika Jumapili hii.
Hizi ni picha za maandamano hayo:



No comments:
Post a Comment