Brazzaville, Gabon. Timu ya Taifa ya Cameroon ‘Simba
Wasiofugika’ imetinga nusu fainali ya mashindano ya Afcon baada ya kuitoa timu
ya Taifa ya Senegal ‘Simba wa Teranga’ kwa jumla ya mikwaju ya penalti 5-4.
Cameroon imeungana na Burkina Fasso ambayo ilikuwa ya kwanza
kutinga nusu fainali baada ya kuifunga Tunisia 2-0.
Nyota anayeichezea Liverpool, Sadio Mane ndiye aliyeiponza
Senegali kwani penalti yake aliyoipiga imepanguliwa vema na kipa wa Cameroon,
Fabrice Ondoa.
Dalili za Ondoa kumnyima Mane usingizi usiku huu zilionekana
ndani ya dakika 90 za mchezo kwani licha ya straika huyo wa Senegal kutafuta
goli, kipa huyo alilinda lango lake kikamilifu na hatimaye mchezo umemalizika
kwa timu hizo kutoka suluhu ya 0-0.
Hata baada ya kuongezwa kwa dakika nyingine 30, Simba hao wa
milima ya Teranga na Simba Wasiofugika walishindwa kufungana hadi walipoingia
kwenye hatua ya mikwaju ya penalti.
Miaka 15 iliyopita, miamba hiyo ya soka ilikutana katika
hatua ya fainali, Cameroon iliishinda Senegal kwa penalti 3-2 na kutwaa ubingwa
wa AFCON kwa mara ya nne huko Bamako, Mali.
No comments:
Post a Comment