Ali Saleh Kiba al maarufu kama Alikiba ni miongoni mwa
wasanii wakongwe na wakubwa Tanzania, Afrika Mashariki na pengine Afrika kwa
ujumla. Ni mshindi wa tuzo zaidi ya 14 kwa mwaka 2016 ikiwezo tunzo kubwa
kabisa za MTV EMA kwa kipengele cha Best African Act.
Kwa mafanikio makubwa aliyoyapata mwaka jana ikiwemo kupata
mkataba mnono wa kampuni kubwa ya muziki duniani yaani Sony Music na kushinda
tuzo zote hizo ndani ya mwaka 2016 ni wazi kabisa kuwa thamani ya Alikiba
imepanda maradufu barani Afrika na pengine kila mfuatiliaji wa muziki Afrika
angependa zaidi kumfahamu Alikiba, kufahamu kazi zake, ni wapi ametoka na wapi
anakwenda.
Sekeseke lilitokea mwaka jana kwenye show ya Mombasa rocks
iliyofanyika mjini Mombasa, Kenya kati ya Wizkid na Alikiba ni moja kati ya
mambo ambayo yalifanya jina la Alikiba lizungumzwe sana barani Afrika haswa
Tanzania, Kenya na Nigeria ambapo mitandao mbalimbali ya Nigeria iliripoti kua
Alikiba anatrend sana nchini Nigeria.
Ushindi wa MTV EMA pia ambao awali alipewa Wizkid kabla
haujatenguliwa na kupewa Alikiba ni mambo yaliyofanya apate attention zaidi
kwenye soko la muziki barani Afrika.
Kutrend ni kitu muhimu sana katika soko la muziki kwa sasa,
wasanii wengi duniani kote hata mpaka Marekani wamekuwa wakitengeneza kiki
kabla ya kuachia kazi zao mpya ili kupata attention. Nafahamu kuwa msanii Alikiba
amekuwa sio muumini mzuri sana wa kiki, lakini kiki kama hizi ambazo
zinajitengeneza zenyewe ni dhambi kubwa kuacha kuzitumia kibiashara sababu kuna
wanaotamani kutrend hata kwa kutembea uchi lakini hawazipati.
Mapema mwaka huu Alikiba alitangaza ratiba ya World Tour
yake itakayoanzia South Africa kisha America na kumalizikia barani Ulaya. Kwa
mujibu wa ratiba kutoka kwenye posters zake alizozipost Instagram Tour yake
inaanza February mwaka huu. Hivyo mpaka ninaandika makala hii zimebaki siku
tatu kufikia mwezi February.
Kati ya sehemu ngumu sana kupenya kimuziki barani basi ni
Afrika Kusini na hii imetokana na ‘wasauzi’ kuthamini sana muziki wao na
haikushangaza licha ya jina kubwa alilojijengea Diamond Platnumz kwenye kiwanda
cha muziki barani Africa aliwahi kaririwa akisema amefanya collaboration na AKA
ili kupenyeza muziki wake África Kusini.
Sasa wasiwasi wangu ni je? Alikiba anategemea kujaza viti
kwa kuitegemea nyimbo ya Aje pekee? Target yake kwenye hii tour ni kuifanya iwe
ya kidunia au analenga waTanzania pekee wanaoishi kwenye nchi husika? Aliahidi
atatoa Aje remix ambayo ni nyimbo aliyoimba na msanii kutoka Nigeria MI Abaga
lakini mpaka zimebaki siku tatu kabla hatujaingia mwezi anaoanza tour hakuna
dalili ya hiyo nyimbo?
Binafsi nilidhani ingekuWa sahihi sana kama angeachia nyimbo
ambayo amesharekodi mama mkongwe Yvonne Chakachaka kwa lengo la kuiteka zaidi
South Africa kibiashara zaidi ili jina lake liwe kubwa nchini humo hata wakati
wa Tour yake angetumia pia na fursa hiyo kufanya media tour kuitambulisha zaidi
hiyo ngoma.
Nadhani si Mimi ila asilimia 98 ya mashabiki hawaridhishwi
na namna ambayo Alikiba amekuwa slow sana na kutojua namna soko la mUziki
linavyoenda na nini linataka. Ni jana kupitia mtandao wa instagram msanii wa
maigizo ambaye pia ni shabiki mkubwa wa msanii Alikiba alipost kipande cha
screenshot kikionesha ujumbe aliotumiwa na shabiki mwingine wa Alikiba DM kua
Ali atapoteza mashabiki wake sababu hawapi raha wanayoitaka, siku zote amekuwa
mtu wa kujiamini na kuwasibirisha mashabiki wake ambao ukweli bila wao
asingekua hapo halipo leo.
Mwaka mpya umeanza kwa kasi kweli kila mtu yuko kasi lakini
naona Alikiba bado yule yule.
No comments:
Post a Comment