YAWEZEKANA ikawa
ni moja ya sababu ya
mvua kuchelewa kunyesha mkoani Iringa tofauti na
ilivyozoeleka miaka mingine
ni kutokana na laana kama
hizi baada ya kikosi
maaalum kinachoongozwa mkuu wa
wilaya ya Iringa Richard
Kasesela kwa kushirikiana na OFM kufanikiw kumkamata kijana Emmanuel Mkiwa (19) kwa tuhuma za kumbaka mara kwa
mara mdogo wake wa
miaka (4)
Afisa maendeleo
ya jamii Manispaa ya
Iringa Josephina Mwaipopo akiwa na mtoto aliyebakwa
Imedaiwa kuwa kijana
huyo ambae ni mwenyeji
wa mtaa wa Omary Matrekta kata ya Mtwivila
katika Manispaa ya Iringa alikuwa akiishi nyumba moja na babake pamoja na wadogo zake watatu
wawili wa kiume na mmoja ni mtoto
huyo wa miaka 4
ambaye alitelekezwa na
mamake mzazi kutokana na mambo ya kifamilia kati yake baba
wa mtoto .
Mashuhuda wa
tukio hilo lililotokea January 16 majira ya saa 2 usiku walimweleza mwandishi
wa OFM Iringa
kuwa kijana huyo mara kwa mara
alikuwa akimbaka mdogo wake
huyo ambae baba mmoja
na mama tofauti kabla ya mtoto
huyo kuwaeleza majirani kuwa
kakake huyo amekuwa akimkandamiza na kijiti sehemu
zake za siri (Akimbaka)
Kutokana na maelezo
ya mtoto huyo ndipo taarifa za
raia wema hao zilipofikishwa kwa mkuu wa
wilaya na OFM na kuamua
kufika katika eneo la tukio na
kufanikiwa kumkamata kijana huyo
na baba mzazi wa watoto hao
Shukuru Mkiwa kwa malezi mabaya
ya watoto.
Akizungumza baada ya
kukamatwa kwa kijana
huyo mkuu wa
wilaya ya Iringa Richard Kasesela
pamoja na kuwashukuru raia
wema kwa
kufikisha taaarifa ya kunyanyaswa
kwa mtoto huyo bado
alitoa wito kwa wananchi wengine ambao
wanataarifa za kunyanyaswa
kwa mtoto yeyote katika
wilaya ya Iringa kutoa taarifa
ili wahusika wakamatwe na
kufikishwa katika vyombo
vya sheria.
Kasesela alisema kuwa
uchunguzi uliofanywa baada ya vipimo katika
Hospitali ya Rufaa ya mkoa
wa Iringa umeonyesha mtoto huyo kashaondolewa usichana wake na
hivyo kulazimika kulazwa kwa
matibabu katika Hospitali hiyo
huku akiahidi kumsaidia mtoto huyo kumsomesha .
Alisema kuwa yawezekana
moja ya sababu ya mvua
kuchelewa kunyesha katika
mkoa wa Iringa ni
pamoja na matukio ya kinyama kama haya ya ubakaji watoto na
kuwa hatakubali kuona
mbakaji anaendelea kuishi uraiani wilaya ya Iringa kwani tayari mkuu
wa mkoa wa
Iringa Amina Masenza kupitia kikao
cha makati ya ushauri ya mkoa (RCC) aliagiza wabakaji wote wasakwe kwa
udi na uvumba na yeye ameanza
kutekeleza agizo hilo.
Japo alisema alishangazwa
na hatua ya baba mzazi wa kijana
huyo kumficha mbakaji ndani na
kudanganya kuwa hayupo wakati
kijana wake alikuwepo ndani hivyo
mzazi huyo kukamatwa pamoja na kijana wake yeye kwa kosa la
kumchifa mharifu na kijana wake kwa kosa la ubakaji .
“Hiki ni kikosi
kamili ambacho kitaendelea kuendesha
misako mbali mbali kwa
kushirikiana na oparesheni Fichua Maovu
(OFM) ya Global Publishers hivyo kwa
yeyote anayejua wapi
mtoto anafanyiwa vitendo vya
kikatili piga simu hii mwandishi wa OFM
Iringa 0754 026 299 tutakufikia ulipo na
kuchukua hatua”
Jeshi la polisi mkoa
wa Iringa kupitia kwa kamanda wa
polisi mkoa (RPC) Julius Mjengi
limethibitisha kukamatwa kwa
mtuhumiwa huyo na kuwa baada ya
upalelezi atafikishwa
mahakamani huku likiwataka
wananchi kuendelea kufichua
waharifu zaidi
No comments:
Post a Comment