Uchunguzi uliofanywa na Samsung kuhusu visa vya simu aina ya
Galaxy Note 7 kushika moto, umebaini kwamba visa hivyo vilitokana na kasoro
kwenye betri.
Kampuni hiyo iliacha kutengeneza na kuuza simu hizo Oktoba
mwaka jana baada ya visa hivyo kuripotiwa kwa wingi.
Simu ambazo zilitolewa upya pia zilikuwa zinashika moto.
Lakini Jumatatu, Samsung imesema tatizo halikutokana na
programu za simu hiyo iliyotarajiwa kutoa ushindani kwa simu za iPhone
zinazotengenezwa na kampuni ya Apple.
Aidha, Samsung wamesema kasoro haikuwa kwenye sehemu
nyingine za simu hiyo ila kwenye betri pekee.
Hatua ya kuzichukua tena simu zote zilizokuwa zimeuzwa
inakadiriwa kuigharimu kampuni hiyo ya Korea Kusini jumla ya $5.3bn (£4.3bn) na
kuathiri pakubwa sifa za kampuni hiyo.
Uchunguzi wa ndani na uchunguzi huru "umebaini kwamba
betri ndizo zilizokuwa chanzo cha moto katika Note 7," Samsung imesema
kwenye taarifa.
Kampuni hiyo imesema kasoro kwenye uchoraji wa muundo wa
betri hizo pamoja na kasoro kwenye mfumo wa utengenezaji wa betri hizo,
zilisababisha betri hizo ambazo ziliundwa na kampuni mbili kuwa na kasoro.
No comments:
Post a Comment