Neymar ndio mchezaji mwenye thamani ya juu barani Ulaya
akiwa na pauni milioni 216 kulingana na utafiti mpya ambao pia unatoa thamani
ya wachezaji kumi walio na thamani ya Yuro milioni 100.
Mshambuliaji huyo wa Barcelona amempiku mchazaji mwenza
katika klabu ya Barcelona Lionel Messi ambaye ana thamani ya pauni milioni 149.
Mchezaji wa pekee kutoka Uingereza aliyeorodheshwa miongoni
mwa wachezaji 10 walio na thamani ya juu duniani ni mshambuliaji wa Tottenham
Harry Kane mwenye thamani ya pauni 122 na Dele Alli mwenye thamani ya pauni
milioni 96.
Paul Pogba ambaye alijiunga na klabu ya Manchester United
kwa rekodi ya kitita cha pauni milioni 89 ana thamani ya pauni milioni 136.4.
Utafiti huo umefanywa na kundi moja la wasomi kutoka CIES.
Walitafuta thamani hiyo kupitia viwango vya uchezaji wa
wachezaji hao, kama vile umri na urefu wa kandarasi.
Pogba ni mchezaji wa pekee aliyeko miongoni mwa 5 bora
ambaye hachezei klabu ya Uhispania huku Antoine Griezman akiwa katika nafasi ya
tatu na thamani ya pauni milioni 132 naye mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez
akiwa wa tano na thamani ya pauni milioni 127.
Kuna wachezaji 42 wa klabu za ligi ya Uingereza miongoni mwa
100 bora akiwemo Eden Hazard wa Chelsea mwenye thamani ya pauni milioni 89,
Anthony Martial wa Manchester United mwenye thamani ya pauni milioni 81, Raheem
Sterling wa Manchester City mwenye thamani ya pauni milioni 75 na Jamie Vardy
wa Leicester City mwenye thamani ya pauni milioni 45.
Kiungo wa kati wa West Ham Michail Antonio anafunga orodha
ya wachezaji 100 wenye thamani ya juu akiwa na thamani ya pauni milioni 31.
No comments:
Post a Comment