Mwana FA anaamini kuwa katika muziki kushindanishwa kwa
wasanii ni kitu ambacho hakiwezi kuepukika. Na katika miaka ya hivi karibuni
ambapo shabiki ana access ya kukosoa, kusifia au kushindanisha, ndio imekuwa
balaa kabisa, lakini hakukwepeki.
“Leo Mwana FA akitoa wimbo mzuri, watakuambia Mwana FA mkali
kuliko fulani na fulani, kuna watu watakuambia MC fulani sababu ametoa wimbo
sasa hivi, wimbo wake mkali basi MC fulani ndio mkubwa kuliko mamcee wote
waliowahi kutokea nchi hii. Kama wanavyosema, opinion sio kitu ambacho mtu
anaweza kushtakiwa kwa kuwa nacho, unless ni za kisiasa ama zina matatizo
kwenye usalama wa taifa na vitu kama hivyo, lakini kila mtu anaruhusiwa kuwa na
zake na hatuwezi kukulazimisha ubadilishe opinion zako,”
FA amesema tatizo pekee katika uhuru huo wa kujieleza na
kuwa na majukwaa mengi ya kutoa maoni, watu ambao hawana uelewa wa kutosha
katika kile wanachokielezea, hupotosha ukweli.
“Mfano halisi ni hili tunalolizungumzia, kuna watu hawajui
muziki, wengine wameanza kusikiliza muziki miaka mitatu minne hii, au pengine
wamesikiliza zamani, lakini wanausikiliza muziki juu juu, hawajui hata nini
kinaendelea, wao wanaenda na hype tu, ngoma itakayohit ndio ngoma yao, msanii
atakayehit ndio msanii bora kwa wakati huo. Kwahiyo watu wa aina hiyo wakitoa
opinion zao unakuta msanii ana mwaka mmoja akalinganishwa na msanii ambaye
ameweza kudumu kwenye game kwa miaka kumi na nne , kumi na tano na wakakuambia
mwenye mwaka mmoja mzuri zaidi,” amesisitiza.
FA anasema kwa ukweli huo, wasanii hawapaswi kuumiza kichwa
sana labda kama na watu ambao wanafahamika kuwa na uelewa mkubwa wa tasnia
wakikumbwa na mafuriko ya hype.
“Haya maoni ya kwamba fulani ndio mcee mkali kuliko mamcee
wote, yanatakiwa yaishie kuwa fulani ana wimbo mkali kuliko nyimbo zote za
marapper zilizotoka kwa wakati huu. Msanii fulani ametoa wimbo mzuri kuliko
nyimbo zote zilizotoka kwa wakati huu. Lakini hatumweki kwamba ndio msanii
mzuri kuliko wote, ndio rapper bora kuliko wote kwa wakati huu, hiyo inakuwa
disrespectful na inatakiwa isitiliwe uzito wowote. Ni kama yale maoni kwamba
‘huo wimbo wa FA wenyewe sijausikia lakini mbaya’, sasa hujausikia wimbo
unakuaje mbaya?”
No comments:
Post a Comment