
Leo January 29 2017 kupitia Funguka ya AzamTV, katibu mkuu
wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amehojiwa na kuzungumzia ishu
mbalimbali ikiwemo za Profesa Lipumba, Zanzibar na maamuzi yake mengine.
Kweli Lipumba alijiuzulu na alipoonyesha nia ya kujiuzulu
tulimfuata kwenda kumuomba sana asiondoke hasa wakati ule tulikuwa tunakabiliwa
na uchaguzi lakini akaendelea na msimamo wake, hakufukuzwa
Lipumba kajiuzulu mwenyewe, amekaa baada ya miezi 10 anaandika
barua kwamba anatengua jambo hili mimi sijawahi kuliona hilo Duniani
Fedha za ruzuku zimekwenda kwenye akaunti ambayo bodi ya
wadhamini, katibu mkuu hawaijui
Ukiingia kwenye siasa lazima ukubali kutukanwa,
kushambuliwa, kufungwa hata kifo, mimi yote nimeshapitia isipokuwa kifo-Maalim
Seif.
Jimbo la Dimani kihistoria ni la CCM na sisi tuliingia
kwenye uchaguzi tukijua tuna kazi kubwa’Ulikosa?
Natarajia muda mfupi ujao nitakuwa Rais wa Zanzibar’
Baada ya kuacha wadhifa safari zote za nje najilipia mwenyewe
na siombi serikalini ingawa nina haki
Hakuna namna yoyote Zanzibar lazima vyama vishirikiane, hii
itawaleta Wazanzibar pamoja
Haiwezekani chama kimoja cha upinzani kuishinda CCM lakini
UKAWA itasaidia

Jecha alisema anafuta uchaguzi ametumia kifungu gani cha
katiba, kama nilifanya kosa kutangaza matokeo kwa nini hawakunipeleka
mahakamani?
Lipumba alidhani akijiuzulu wengi watamfuata lakini
haikuleta athari CUF, uchaguzi 2015 tulishinda majimbo 10 TZ bara,
Mtu akijiuzulu atumpi tena nafasi, katiba yetu hairuhusu
hivyo, Mtu anajiuzulu halafu anarudi unafikiri anarudi kwa mema
Siwezi kukiacha chama cha CUF wala sijafikiria kuunda chama
kingine.
No comments:
Post a Comment