
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha,
Augustino Rwezile, leo, anatarajia kuwasomea hoja za awali Mbunge wa Arusha Mjini,
Godbless Lema na mkewe, Neema katika
kesi inayowakabili ya kumtukana Mkuu wa mkoa huo, Mrisho Gambo.
Hoja hizo ilikuwa wasomewe Novemba 15, 2016 lakini zilikwama
kusomwa kutokana na Lema kuugua ghafla na Wakili wa Serikali, Elizabeth Swai
kumuomba hakimu kutumia busara ya Mahakama kuisogeza mbele kesi hiyo kutokana
na hali ya mbunge huyo.
Lema bado anasota rumande kwa siku 76 tangu Novemba 2, mwaka
jana baada ya kukosa dhamana katika kesi inayomkabili ya tuhuma za kutumia
lugha ya uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli.
Kutokana na sababu hiyo, Hakimu Rwezile pia amwahirisha kesi
ya kuhamasisha maandamano ya Ukuta inayomkabili mbunge huyo na ile ya kumtumia
ujumbe mfupi wa maneno Gambo unaodaiwa kuwa na matusi hadi leo.
No comments:
Post a Comment