
PAA za madarasa sita ya Shule ya Sekondari Kisumwa iliyopo
katika Tarafa ya Suba mkoani Mara pamoja na nyumba za walimu na choo,
zimeezuliwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo.
Mvua hiyo iliyonyesha mwishoni mwa wiki, pia imeharibu
nyumba na mazao ya wakazi wa vijiji vya Kisumwa na Mara Sibora mkoani Mara.
Akizungumza na Nipashe mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Charles Chacha, alithibitisha
kuwapo kwa tukio hilo.
Chacha alisema mvua hiyo ilinyesha wilayani Rorya ikiwa ni
baada ya zaidi za mwezi mzima ikikumbwa na ukame.
Alisema mvua hiyo iliyokuwa imeambatana na upepo mkali,
iliezua paa za madarasa sita, nyumba ya mwalimu na choo katika Shule ya
Sekondari Kisumwa.
Kadhalika, Chacha alisema mvua hiyo pia iliharibu mazao na
baadhi ya nyumba za wakazi wa vijiji vya Kisumwa na Mara Sibora.
Alisema Kamati ya Maafa chini ya Mkuu wa Wilaya ya Rorya,
Saimon Chacha, itafanya tathmini ya mali iliyoharibika katika shule hiyo na kwa
wakazi wa vijiji hivyo.
Aidha, Mkurugenzi huyo amewahimiza wananchi wa Wilaya ya
Rorya kuzitumia mvua zinazoendelea kunyesha kupanda mazao yanayokomaa kwa muda
mfupi na yanayovumilia ukame.
No comments:
Post a Comment