Simba ni mnyama ambaye hulka yake ni kulinda himaya yake, na
ni maarufu kwa jinsi anavyotumia nguvu kuhakiksha anapata akitakacho wakati
wowote pahali popote. Hivyo huogopwa na kuheshimiwa na wanyama wenzake maana
yeye huwa hana mzaha a biashara zake ilimradi tu ahakikishe jamii yake
inafaidika kutoka kwa windo lake.
Huenda sifa za mnyama huyu ndizo zilizopelekea CEO wa WCB
Naseeb Abdul Juma aka Diamond Platnumz kujiongezea jina la Simba kama moja aka
zake. Kwa ubunifu wake wa hali ya juu, star huyo wa wimbo Salome hasiti kuwatoa
kijasho wasanii wenzake kwa kasi zake, si kimziki pekee bali pia kibiashara.
Wakati wengi wakitaka kumpiku kisanaa kwa kutoa hits na
video kali ili kuvutia mashabaki, yeye anazidi kutumia hela anazoingiza kupitia
muziki wake kwa show anazopiga hapa Afrika hadi Ulaya kupanua himaya yake ya
WCB kwa kujenga na kununua nyumba za kifahari ikiwemo moja nchini Afrika
Kusini.
Nina hakika Afrika Kusini kama vile ilivyo hapa Afrika
Mashariki kuna baadhi ya wasanii tajika ambao bado wanaishi katika nyumba za
kupanga. Inatisha sana ukiona msanii kutoka nchi ya kigeni kama Tanzania
akimiliki nyumba ya kifahari kwa thamani ya zaidi ya milioni 400 iliyopo katika
jiji la Pretoria.
Juzi tu, meneja wake Sallam alitangaza kuingia sokoni wakati
wowote lwa manukato ya Chibu Perfume ambayo mwaka jana 2016 sample zake
zilionyeshwa kwa mara ya kwanza nakuwapa hamu ya kuzitumia mashabiki wake kote
barani Afrika.
Wakati mashabaki wake wakiwa katika harakati za kushangilia
ujio wa Chibu Perfume ndani ya soko la Afrkca, siku tano zilizopita Baba Tiffa
alirusha video kupitia kichunusi chake cha Instagram akiwa anaonyesha furaha
baada ya kusaini (endorsement deal ) ya mamilioni ya pesa japo hakuweka wazi
kama deal hiyo ilikuwa imetoka kwa kampuni gani.
Baraka hizi zote lazima zinawapa homa na kichefuchefu
wasanii wengi Afrika, kwani kila mmoja anapania kufikia upeo wa mafanikio hayo.
Umaarufu wake barani Afrika na nje, unamfanya kuwa na kila sababu ya kumiliki
aka yake ya Simba.
Mwaka ukiwa bado mchanga, ameanza na mbwembwe za kuuonyesha
ulimwengu kuwa pia yeye ni star katika uwanja wa biashara na vigezo vya
ujasirimali vimejitokeza wazi. Heko Chibu kwa juhudi unazopiga wewe. Wewe ni
msanii kioo cha jamii, waonyeshe njia nzuri vijana wasiishie kwenye lindi la
dawa za kulevya.
No comments:
Post a Comment