Kimaira: Kiini tete cha binadamu na nguruwe chakuzwa Marekani. - boazmwakasege.com

MADA MOTO

Friday, January 27, 2017

Kimaira: Kiini tete cha binadamu na nguruwe chakuzwa Marekani.

Kiinitete

Viini tete ambavyo ni 0.001% binadamu na sehemu iliyosalia ni nguruwe, vimekuzwa na wanasayansi nchini Marekani.

Hicho ni kisa cha kwanza kwa viumbe ambao ni mseto wa binadamu na viumbe wengine kuzalishwa kwa kuunganisha sehemu kutoka kwa binadamu na viumbe vingine.
Lengo limekuwa kujaribu kubaini iwapo inawezekana viungo vya binadamu kukuzwa kwenye wanyama.

Watoto kuzaliwa na wazazi watatu Uingereza
Nyota wa filamu India abeba nguruwe kwenye benki
Hata hivyo, makala ya kisayansi iliyoandikwa kwenye jarida la Cell inaonyesha shughuli hiyo ina changamoto nyingi.

Makala hiyo imeelezwa kuwa "ya kusisimua sana" na watafiti wengine.

Ilii kuunda kiini tete kama hicho ambacho kimepewa jina kimaira (Chimera), - ambaye ni mnyama katika hadithi mwenye kichwa cha simba, mwili wa mbuzi na mkia wa nyoka, atokaye moto kinywani - wataalamu walitumia seli tete (seli zinazoweza kukua kuwa seli za aina yoyote mwilini) na kuziweka ndani ya kiini tete cha nguruwe.

Seli

Kiini tete hicho - ambacho sasa kimechanganyikana seli za binadamu na nguruwe - kiliwekwa ndani ya nyumba ya uzazi ya nguruwe jike na kukaa kwa mwezi mmoja.

Shughuli hiyo hata hivyo ilikuwa na changamoto nyingi na kati ya viini tete 2,075 vilivyowekwa ndani ya nguruwe, ni viinitete 186 vilivyokuwa hadi siku ya 28.

Hata hivyo, kulikuwa na dalili za matumaini kwamba seli za binadamu zilikuwa bado zinakuwa, ingawa ziliunda sehemu ndogo sana ya viungo vya mwili kwenye kiinitete hicho kilichochanganyikana seli za nguruwe na binadamu.

No comments:

Post a Comment