Mchezaji wa mpira wa kikapu nchini New Zealand Akil Mitchell
amesema anapata nafuu baada ya jicho lake kutoka alipokuwa uwanjani akicheza.
Mitchell huchezea klabu ya New Zealand Breakers, na alikuwa
mjini Auckland kucheza mechi ya NBL ya Australia Alhamisi usiku kisa hicho
kilipotokea.
Mchezaji wa timu pinzani aliingiza kimakosa kidole ndani ya
tundu la kishimo cha jicho na ghafla jicho lake likatoka nje.
Mchezaji huyo mzaliwa wa Marekani alianguka sakafuni akiwa
ametumia mikono yake kufunika jicho lake la kushoto na akakimbizwa hospitalini.
"Kwa viganja vya mkono wangu, nilihisi mboni ya jicho
ikiwa nje na kukaa upande mmoja wa uso," aliambia Radio Sport ya New
Zealand.
"Bado jicho hilo lilikuwa linaona."
"Nakumbuka nikifikiria, bwana we ... hii ni hali mbaya,
lakini nilihisi kwamba lilikuwa jambo la kushangaza na hapo ndipo niliingiwa na
wasiwasi kiasi
Mchezaji huyo wa miaka 24 anasema anakumbuka kusikia
mashabiki na wachezaji wake wakiingiwa na wasiwasi.
Alidhani hangeweza kuona tena na kwamba uchezaji wake ulikuwa
umefikia kikomo.
"Nilipoingizwa kwenye gari la kubeba wagonjwa walinipa
dawa za kupunguza maumivu na matoneo kadha ya dawa yenye chumvi machoni na
nikasakia mboni ya jicho ikirudi ndani, jambo ambalo pia lilikuwa la
ajabu."
"Najihisi mwenye furaha sana kuweza kufunga na kufungua
macho tena, ni jambo la kushangaza."
No comments:
Post a Comment