Mshambuliaji wa klabu ya Nice nchini Ufaransa Mario
Balotelli anasema kuwa alikuwa mwathiriwa wa ubaguzi wa rangi wakati wa mechi
ya Ijumaa dhidi ya Bastia.
Mchezaji hyo wa zamani wa Liverpool mwenye umri wa mika 26
alichapisha katika mtandao wa kijamii akisema, ni jambo la kawaida kwamba
wafuasi wa Bastia hufanya makelele ya tumbili kwa mechi yote na hakuna mtu
katika idara ya adhabu anayechukua hatua?
''Kwa hivyo ubaguzi wa rangi ni sheria halali nchini
Ufaransa? Ama ni Bastia pekee? Soka ni mchezo mzuri lakini watu kama wafuasi wa
Bastia wanaharibu.Ni aibu kubwa''.
Balotelli alicheza dakika 90 aliporudi uwanjani baada ya
kuhudumia marufuku katika mechi iliotoka sare ya 1-1 huko Corsica.
Ujumbe huo uliotumwa katika mtandao wa Instagram ulisambazwa
na Nice katika mtandao wa Twitter wa klabu hiyo.
Jopo la adhabu la ligi ya Ufaransa ambalo hutoa maamuzi
halijatoa tamko lolote.
Balotelli amefunga mabao 10 katika mechi 15 tangu kujiunga
na Nice katika uhamisho huru kutoka Liverpool mwezi Agosti ,miaka miwili baada
ya uhamisho wa pauni milioni 16 kuelekea Anfield.
Chanzo: sky sport
No comments:
Post a Comment