
Utendaji wa
JPM waipaisha sekta ya utalii Uchambuzi wa kina wa hali ya mambo katika sekta
moja muhimu ya utalii, eneo linaloiingizia Serikali takribani asilimia 25 ya
fedha za kigeni, unaonesha, pamoja na kelele za hivi karibuni, watalii wengi
wameongezeka nchini hasa katika kipindi cha Julai mpaka Agosti mwaka huu ikiwa
ni ongezeko la asilimia 11.
Uchunguzi
zaidi umeonesha kuwa watalii wengi waliokuja nchini au wanaofikiria kuja nchini
hawajaguswa na ongezeko hilo la kodi zaidi ya kujali aina ya vivutio vilivyoko
nchini, hali ya amani na wapo wanaovutiwa pia na utawala wa Rais John Pombe
Magufuli ambaye anasikika duniani kote hivyo wanakuja kuona hali ya siasa
nchini.
Katika
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, takwimu za watalii waliotembelea hifadhi
hiyo, kwa kipindi cha Juni hadi Agosti, 2015 na Juni hadi Agosti, 2016 nako
zinaonesha ongezeko.
“Kwa
kulinganisha idadi ya watalii waliotembelea Hifadhi ya Ngorongoro kwa miezi
mitatu (Juni-Agosti 2015) na mwaka Juni hadi Agosti,2016, inaonekana kuwa idadi
ya wageni imeendelea kuongezeka hivyo mapato pia yameongeza.
“Kwa mantiki
hiyo hadi sasa utekelezaji wa kodi mpya haujaathiri mapato na haijawa kikwazo
bado kwa watalii kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro,” inasema taarifa ya hali ya
utalii nchini ambayo gazeti hili limeiona sehemu yake.
Tayari
watalii wenyewe na wataalamu wa sekta hiyo waliokuja nchini kwa wingi licha ya
kodi kuongezeka, ripoti hiyo ya kina inaainisha, wengi hawakuonekana
kubabainishwa na kodi hiyo:
“Watalii
waliohojiwa kwenye malango na mahoteli walionyesha kutoelewa kuwa VAT imeanza
kutozwa na baadhi walishangaa kwamba Serikali haikuwa inatoza kodi fedha
zilizokuwa zinalipwa na watalii waingiapo Hifadhini,” inasema ripoti hiyo.
Akiandika
katika makala yake iliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza Why VAT will not kill
hotels, tourism na kuchapishwa na gazeti moja la kila siku nchini, mmoja wa
walimu wanaofanyakazi nchini Australia na mtalii wa mara kwa mara kuja Tanzania
na sehemu nyinginezo Afrika, Sabine Barbara anasema:
“Hali ya
kisiasa ya nchi inaweza kuwa na athari zaidi kwa watalii kuliko kuongezeka kwa
ada za kuingia katika mbuga za wanyama….juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano
zitapimwa unapofika mwisho wa mwaka kuliko kuanza kuwatisha watu hivi sasa kuwa
kodi zitapunguza watalii.”
Takwimu hizi
zinakuja wakati ambapo wiki iliyopita akizungumza katika kipindi cha
TUNATEKELEZA, kinachorushwa na TBC1, Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof.
Jumanne Maghembe akidokeza na kuthibitisha kuwa kodi mpya ya VAT haikuwa
imeathiri idadi ya watalii wala mapato ya nchi.

Akizungumzia
jana na gazeti hili kuhusu kuongezeka kwa watalii licha ya wasiwasi wa awali wa
kodi hiyo ya VAT, Meneja Mawasiliano wa TANAPA, Bw. Paschal Shelutete, alisema
ni kweli kuna ongezeko hilo na wao walilitarajia.
“Ni kweli
kwamba watalii wameongezeka kuja kutembelea hifadhi zetu na vivutio vingine vya
nchi. Hakuna mtalii anayeweza kushindwa kuja nchini kwa sababu ya kutakiwa
kulipa kodi. Bahati nzuri wenzetu wanautamaduni wa kuheshimu sana kodi na ndio
maana hawajastushwa na kodi hiyo,” alisema.
Takwimu
hizi, hasa katika kuelekea mwaka mmoja wa uongozi wake, zinampa Rais Magufuli
nguvu ya kuendeleza zaidi utawala wake unaojikita katika kuhakikisha kodi za
Serikali zinalipwa ili kuiongezea Serikali mapato kwa lengo la kufikia azma ya
kujitegemea.
Itakumbukwa
kuwa Julai mwaka huu Serikali ilianza kutekeleza kodi mpya ya ongezeko la
thamani (VAT) katika sekta ya utalii, hatua iliyopingwa na wadau wa sekta hiyo
kuwa ingeathiri idadi ya watalii wanaokuja nchini.
Miezi miwili
baadaye, takwimu zinathibitisha kuwa ongezeko hilo la kodi ambalo Rais Magufuli
mwenyewe amepata kulitetea, tofauti na mawazo ya wengi, halijaathiri, na badala
yake sababu nyingine kama vivutio vilivyopo nchini na hali ya amani na utulivu
vimeendelea kuifanya Tanzania iwe na mvuto zaidi kwa watalii.
Takwimu
ambazo kutoka kutoka vyanzo mbalimbali Serikalini, sekta binafsi na kwa wadau
wa utalii wenyewe, zinathibitisha kuwa wakati kwa mwaka mzima wa 2015 idadi ya
watalii waliongia nchini ilikuwa 1,1376,182 idadi hiyo imeongezeka mwaka huu.
Takwimu hizo
zinaonesha kuwa kwa kuangalia ulinganifu wa takwimu za mwaka jana kipindi kama
hiki na mwaka huu, takwimu za Hifadhi za Taifa (TANAPA), zinaonesha idadi ya
watalii wote katika kipindi cha Juni-Julai 2016 imeongezeka kwa sana.
Ongezeko
hilo pia limeongeza mapato yatokananyo na viingilio hifadhini ambapo
yameongezeka kwa wastani wa asilimia 19.7 huku mapato yatokanayo na vyanzo
vingine yakiongezeka kwa wastani wa asilimia 13.
Julai mwaka
huu, Serikali ilianzisha kodi ya VAT ambayo itakuwa ikikatwa kwenye huduma za
uongozaji watalii, kuvinjari (safari) na ada za viingilio (park fees)
hifadhini. Huduma za malazi zilishakuwa zikitozwa kodi hiyo tangu awali.
“Baada ya
miaka ya 10 sekta ya utalii kufaidika na msamaha huo, Serikali iliona sekta
imeimarika na ni vema sasa ichangie zaidi katika mapato ya nchi moja kwa moja
kwa kuondoa msamaha huo,” anasema mtaalamu mmoja wa masuala ya kodi katika
sekta binafsi na kuongeza:
“Hivyo,
msamaha huo ulifutwa kupitia Finance Act ya mwaka 2016 (Juni). Takwimu am,bazo
hata sisi tunazo zinaonesha katika kipindi hiki cha Julai na Agosti, 2016
ambapo huduma za utalii zimeanza kutozwa VAT hapakuwa na athari ya mapato kwa
Serikali.”
Na Mwandishi
Wetu, Gazeti la Majira, Sept., 13, 2016
WAKATI
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli ikielekea
kutimiza mwaka mmoja Novemba mwaka huu, mageuzi makubwa anayoyafanya, staili
yake binafsi ya uongozi na mafanikio katika kulinda misingi ya amani
vimeendelea kuwavutia wageni wengi duniani.
Katika
kuelekea mwaka mmoja wa Serikali ya Magufuli, wachambuzi wanaweza kutazama
utawala wake kwa namna tofauti kwa kuangalia na kuzingatia nyanja za uchumi,
siasa, jamii na teknolojia.
Uchunguzi wa
unaonesha kuwa sera na staili ya uongozi wa Rais Magufuli hasa katika nyanja za
uchumi zimeanza si tu kuwavutia wageni kutoka nje lakini pia kuipatia nchi
mapato yaliyokuwa yakipotea awali.
No comments:
Post a Comment