
Msanii wa
Bongo Fleva Mr. Blue ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa 'Mboga
Saba' amefunguka na kusema kuwa saizi yeye ni mtu mzima anaangalia maisha yake
na familia yake hivyo hawezi kurudia matapishi ambayo tayari alishakwisha
yatapika.
Mr Blue
alisema haya kupitia kipindi cha eNewz ya EATV alipokuwa akifafanua juu ya
taarifa zilizokuwa zimezagaa mtaani kuwa alimpigia simu aliyekuwa mpenzi wake
wa zamani Naj ndipo hapo aliposema hawezi kurudia matapishi aliyokwisha
yatapika.
"Niliongea
na Baraka The Prince alisema kuwa wao hawakufanya hilo jambo, lakini kama
wangekuwa ni wao lazima ningetafuta njia ya kuwashikisha adabu maana huko ni
kuharibiana. Mimi saizi nimeshakuwa mtu mzima siwezi kurudia matapishi ambayo
nilishakwisha yatapika mwanzo' alisema Mr Blue.
No comments:
Post a Comment