
Hi guys,
niaje?
Ni miezi
miwili sasa tangu nimeacha kazi kampuni ya zamani, na sasa nipo kwenye kampuni
nyingine, hii kazi mpya nimetafutiwa na Boss wangu ambae ndie mkuu wa idara
yetu, nimepanda cheo kidogo, kule nilikuwa Karani na huku kupya mimi ni
Supervisor.
Sasa huyu
Boss alieniingiza kazini nimekua na urafiki nae tangu nimeingia hapa, kitu
kinachonikwaza ni mwenendo wa huyu Boss wangu, yaani nimekua kama mtumwa,
wakati wote anataka tufanye ngono, jioni wakati wa kuondoka anataka tubaki
ofisini kwake, najikuta nafika home saa tatu hivyo kumkuta Mr wangu amesharudi
Muda, inakua ugomvi, inabidi nimdanganye kuwa kazi mpya imekua too demanding
kwangu, nachelewa kutoka.
Weekend ni
hivyo hivyo, inabidi nisingizie home kuwa tunatakiwa kazini hata Jumapili,
nimejikuta naishi kama mtumwa kwa sababu ya hii kazi aliyonipa huyu Boss,
maneno maneno yamekua mengi hapa kazini miongoni mwa Staff wenzangu kuhusu
mwenendo wangu na huyu Boss, nina wasi wasi maneno haya yanaweza kumfikia Mr
wangu ikawa shida.
Natamani
kuirudia ile kazi yangu ya awali, kazi hii mpya napata mshahara mzuri lakini
nimekua kama mtumwa, wakati mwingine nikionesha dalili za kumgomea kubaki jioni
anakua mkali na kuanza vitisho kwamba eti '' unasahau nani kakuweka hapo
''Inabidi tu nishiriki nae ingawa sipendi.
Naombeni
ushauri nifanyeje?
No comments:
Post a Comment