
KUNA TAARIFA
KUWA waasi wa Mai Mai wamewateka madereva wa Tanzania watano na kuchoma baadhi
ya magari. Wanadai usd 4000 kwa kila Dereva amasivyo watawapiga risasi. Wametoa
deadline ya majeshi kuondoka pia.
Chama cha
Wamiliki wa Magari ya Mizigo nchini Tanzania (TATOA) kinaripoti kwamba, waasi
wa Mai Mai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wamewateka nyara
madereva wa Tanzania na kuchoma baadhi ya magari ya mizigo. Waasi hao wanadai
dola za Kimarekani elfu nne (karibu shilingi za Kitanzania milioni tisa) kwa
kila dereva ama sivyo watawapiga risasi madereva wote. Pia waasi hao wametoa
siku ya mwisho (deadline) ya majeshi yanayolinda amani nchini humo kuondoka.
TATOA
inasema imezungumza na mmiliki wa kampuni ya Simba Logistics, Mzee Azim Dewji
ambaye amethibitisha taarifa hizi na pia balozi wa Tanzania DRC pamoja na
Wizara ya Mambo ya Nje tayari serikali inashughulikia suala hili. Jumla ya
magariyaliyotekwa ni 12 kati ya hayo magari 8 ya Tanzania na 4 ya Kenya. Magari
4 ya Tanzania yamechomwa moto na madereva wote walichukuliwa na waasi lakini
bahati nzuri madereva wawili wa Tanzania walifanikiwa kuwatoroka. Tukio hilo
limetokea sehemu inaitwa Kasebebena na Matete, wastani wa kilomita 30 kutoka
mji wa Namoya.
TATOA
inawashauri wanachama waliopakia mzigo kuelekea huko kuwasiliana na madereva
wao ili wasitishe safari, kusubiri taarifa ya hali ya usalama kutolewa.
Mai Mai Kata
ni kundi la waasi nchini DRC ambalo linadai kupigania uhuru wa jimbo la
Katanga, na linaongozwa na Gédéon Kyungu Mutanga, ambaye aliunda kundi hilo
mara tu alipotoroka kutoka gerezani mwaka 2011.

Tumezungumza
na mmiliki wa kampuni ya Simba Logistics Mzee Azim Dewji amethibitisha taarifa
hizi na tayari tumezungumza na balozi wa Tanzania DRC pamoja na wizara ya mambo
ya nje tayari serikali inashughulikia swala hili. Jumla ya gari zilizotekwa ni
12 kati ya hizo gari 8 za Tanzania na 4 za Kenya.
Gari 4 za
Tanzania zimechomwa moto na madereva wote walichukuliwa na waasi lakini bahati
nzuri madereva wawili wa Tanzania walifanikiwa kuwatoroka. Tukio limetokea
sehemu inaitwa Kasebebena na Matete kilometer 30 kutoka mji wa Namoya.
Tunawashauri
wanachama waliopakia mzigo kuelekea huko kuwasiliana na madereva wao wasitishe
safari ili kusubiri taarifa ya hali ya usalama kutolewa.
Tutazidi kuwapatia
update information.
No comments:
Post a Comment