Waasi hao
mbali na kuwateka madereva hao wametoa saa 24 kuanzia juzi saa 10 jioni walipwe
fedha kiasi cha Dola za Marekani 4,000 kwa kila dereva ili waweze kuwaachia.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga, alisema waasi hao
wametishia kuwaua mateka hao endapo hawatalipwa kiasi hicho cha fedha hadi
kufikia jana saa 10 jioni.
Mindi
alisema katika tukio hilo, madereva wawili wa Kitanzania walifanikiwa kutoroka
na ndiyo waliosaidia kutoa taarifa kuhusu tukio hilo.
“Serikali
imepokea taarifa za kutekwa kwa malori 12 katika eneo la Namoyo Jimbo la Kivu
Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, jana (juzi) Septemba 14, 2016. Kati
ya malori hayo manane yanamilikiwa na mfanyabiashara wa Kitanzania, Azim Dewji
na mengine yanamilikiwa na wafanyabiashara kutoka Kenya.
“Kwa taarifa
zilizopatikana watekaji ni kikundi cha waasi cha Mai Mai ambao baada ya
kuyateka magari hayo, waliwashusha madereva na kuwapeleka porini na kisha
kuteketeza kwa moto malori manne ambayo yote ni ya Dewji.
“Waasi hao
wametoa saa 24 kuanzia jana saa 10 jioni walipwe fedha kiasi cha Dola za
Kimarekani 4,000 kwa kila dereva ili waweze kuwaachia,” alisema Mindi.
Alisema
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
imeshachukua hatua za awali za kuwasiliana na Serikali ya DRC ili kuhakikisha
kuwa madereva hao wanaachiwa haraka iwezekanavyo wakiwa salama kabisa.
Alisema
tukio la aina hiyo ni la pili kutokea ambapo katika mwaka jana masheikh kutoka
Tanzania walitekwa nchini DRC lakini kwa ushirikiano wa Serikali hizo mbili
juhudi ziliweza kuzaa matunda na masheikh hao kuachiwa huru bila madhara
yoyote.
“Serikali
ingependa kuushauri umma wa Watanzania hususan wafanyabiashara kuomba taarifa
ya hali ya usalama kwa maeneo yenye matatizo ya kiusalama kama Mashariki ya
Kongo hususan Kivu ya Kusini kabla ya kusafiri kwenda maeneo hayo,” alisema
Mindi.
CHANZO: BOngo5
No comments:
Post a Comment