
Ripoti
kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC zinasema kuwa wanajeshi wamepata
miili ya takriban raia 30 waliouawa katika shambulizi mashariki mwa taifa hilo.
Msemaji wa
jeshi Mark Azuray ameambia shirika la habari la AFP kuwa mauaji hayo yalitokea
katika mji wa Beni nyakati za usiku.
Wanajeshi
wanashuku kuwa kundi la wanamgambo la ADF lilitekeleza mauaji hayo.
ADF ni kundi
la kujihami lililo na asili yake nchini Uganda, na linaendeleza shughuli zake
karibu na mpaka.
SOMA CHANZO CHA BIFU LA VERA NA HUDDAR, BONYEZA HAPA CHINI.
No comments:
Post a Comment