
Mrembo
kutokea pande za Mombasa nchini kenya, Vera Sidika ametoa sababu ya kuwa na
bifu na mlimbwende mwenzake wa nchini humo, Huddah Monroe, bifu ambalo limeteka
vyombo vya habari kwa muda mrefu
Akifunguka
kwenye FNL ya East Africa Tv na Radio, Vera Sidika amesema wakati yeye akiwa
Mombasa, Huddah Monroe tayari alishakuwa maarufu jijini Nairobi, lakini
alipoenda ingawa walianza kwa kuwa marafiki, lakini baadaye Huddah alionyesha
kutopenda uwepo wa Vera jijini Nairobi, kwani alihisi anamchukulia nafasi yake
kwenye kazi.
"Bifu
ambayo yeye anayo ilikuwa yeye amekuwa Nairobi na tayari alishakuwa star, na
mimi nikatoka Mombasa nikaja Nairobi, ikawa kama nimeingilia career yake, ikawa
anaaza bifu leo, anaanza kesho sasa inachosha, sasa mi nasemaga mambo kama hayo
sitaki lakini anayaleta tu", alisema Vera Sidika.
Vera
aliendelea kusema kuwa kitendo hicho yeye hakipendi, hasa pale inapofikia hatua
ya kuchafuana kwenye mitandao kwa kutoleana habari za uongo, akitolea mfano wa
hivi karibuni wa Hudda kumtangaza kuwa yeye ni muathirika wa Ukimwi.
No comments:
Post a Comment