
MWANAMUZIKI
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amejikuta akiwatibua baadhi ya ndugu zake huku
wengine wakimuita mchafu kutokana na kitendo cha kumpachika mimba mpenzi wake
Zarinah Hassan ‘Zari’ kisha kuwepo madai kuwa ‘amewajaza’ pia mamodo Hamisa
Hassan ‘Mobeto’ na Irene Hilary ‘Lynn’,
Ijumaa lina
habari kamili. Mmoja wa ndugu wa karibu wa Diamond aliyeomba hifadhi ya jina
lake alisema kuwa, familia imeshtushwa na madai kuwa kijana wao huyo mbali na
kwamba Zari a.k.a Mama Tiffah ni mjamzito, amewapa mimba tena Mobeto na Lynn.
gazeti la risasi:

ILIKUWAJE?
Miezi kadhaa nyuma, yaliibuka madai kuwa Zari ni mjamzito lakini Diamond
amekuwa mgumu kulizungumzia hilo licha ya hivi karibuni mazazi mwenziye huyo
kutundika picha akionesha kitumbo chake kilichodhihirisha kuwa ndani yake kuna
kiumbe.
LYNN NAYE
Huku mashabiki wa Zari ‘Team Zari’ wakionesha furaha ya staa wao ‘kumshika’
mwanamuziki huyo kwa kumbebea ujauzito mwingine, zikaibuka taarifa nyingine
kuwa, modo wa Wasafi Classic Baby (WCB) Lynn naye ana mimba ya jamaa huyo.
Ikadaiwa kuwa, kubeba ujauzito kwa Lynn kumekuja baada ya yeye na Diamond kuwa
kwenye uhusiano wa siri huku mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ akidaiwa
kujua kila kitu na kubariki ujio wa mjukuu mwingine.
MIMBA YA
MOBETO
Katika kile
kilichoonesha kuwachefua baadhi ya wanandugu, hivi karibuni yakaibuka madai
kuwa, mwanamitindo Mobeto naye ana mimba na mhusika ni baba Tiffah. Taarifa
hizo zimeonesha kuwashitua wengi akiwemo mama mzazi wa modo huyo, Shufaa
Lutigunga ambaye alipoongea na mwandishi wetu alisema kuwa, amezishangaa ila
anayeweza kueleza ukweli ni Mobeto. Jitihada za kumpata modo huyo ili
kuzungumzia madai hayo hazikuzaa matunda licha ya kwamba aliwahi kuongea na
gazeti hili na kukanusha madai yaliyokuwa yamezagaa kuwa anatoka na Diamond.

FAMILIA YA
DIAMOND ‘YAMAINDI’
Kufuatia madai hayo, ndugu wa karibu wa
Diamond aliyeongea na gazeti hili alisema kuwa, hivi karibuni familia ilikaa
kikao kujadili mambo ya kifamilia lakini pia wakaonesha kukasirishwa na taarifa
ya Diamond kuwapachika mimba wasichana watatu. “Hilo la madai kuwa Diamond
amewapa mimba wanawake watatu licha ya kwamba hatuna uhakika nazo, zimetuchefua
sana, zimetufanya tumuone Diamond ni mchafu au kwa maana nyingine ni mchafuzi.
“Nasema hivi kwa sababu, haiwezekani iwe amempa mimba Zari halafu wakati huohuo
awe amempa tena Lynn na Mobeto, sisi kama familia tutaficha wapi nyuso zetu
wakijifungua? “Ishu hiyo imemfanya kila mtu
kwenye
familia awe muoga, kwani pamoja na hayo yote kutokea, kubwa wanalohofia ni
namna watakavyomwangalia Zari (wifi yao), sasa wakijifungua sijui watamjibu
nini au wataweka wapi sura zao. “Hapa ninavyokwambia mama Diamond na Esma
hawaongei vizuri na Zari kufuatia kuendelea kuwahisi wao ndiyo kikwazo kikubwa
cha kumuunganisha Diamond na warembo hao,” kilidai chanzo hicho.
DIAMOND HUYU
HAPA
Gazeti hili
baada ya kupenyezewa taarifa hizo lilimtafuta Diamond ili kumpa nafasi ya
kulizungumzia kinagaubaga suala hilo, alipopatikana alisema kwamba yote
yanayozungumzwa ni maneno ya watu na hakuna hata moja la kweli. “Hakuna hata
moja la ukweli, mwenyewe najionea kwenye mitandao kama nyinyi, kwani ‘social
network’ kila mmoja ana uhuru wake wa kuongea anachokiwaza na siwezi kuwafuata
na kuwauliza. “Kwa hilo sina la kuongea zaidi maana naona ni mambo ya kipuuzi
tu ambayo siwezi kuyapatia nafasi yoyote kwangu, naona tuachane nayo tu,”
alisema Diamond.
TUJIKUMBUSHE
KIDOGO Diomond amekuwa na skendo kibao za ku-date na wasichana mbalimbali
wakiwemo mastaa ambapo mbali na Zari, Mobeto na Lyn, jamaa huyo aliwahi pia
kutoka na Wema Sepetu, Jokate Mwegelo, Jacqueline Wolper, Upendo Mushi, Penniel
Mungilwa ‘Penny’, Aunt Ezekiel na wengineo.
CHANZO:
RISASI JUMATANO
No comments:
Post a Comment