KAMISHNA wa Sekretarieti
ya Maadili kwa Viongozi wa Umma, Jaji mstaafu Salome Kaganda, amewataka
viongozi wastaafu kuacha kutoa siri za serikali kwani bado wapo kwenye kiapo na
kuonya wakikaidi, watachukuliwa hatua.
Bila
kuwataja kwa majina wala siri walizotoa, Jaji Kaganda alisema: “Tusiweke
maslahi binafsi mbele kwa kutoa siri za mikataba kwa kuangalia manufaa binafsi,
jambo ambalo limelifikisha taifa pabaya. Viongozi wastaafu wafunge midomo yao
kwani bado wako ndani ya kiapo hata kama wamestaafu.”
Jaji Kaganda
alisema wapo wastaafu ambao wameingia kwenye nyanja mbalimbali ikiwamo siasa,
ambapo hutumia majukwaa kutoa siri za serikali na kwamba wanapaswa kukumbuka
wanaweza kuchukuliwa hatua za kisheria.
No comments:
Post a Comment