
Mwanamuziki
Mwana FA amefunguka na kuwataja wasanii wawili ambao yeye siku zote amekuwa
akiwakubali kutokana na uwezo wao na kazi kubwa waliyoifanya katika muziki wa
Hip Hop Tanzania kiasi cha kuwafanya watu waamini muziki huo siyo uhuni bali ni
kazi.
Mwana FA
kupitia kipindi cha Friday Night Live (FNL) kinachorushwa na EATV alisema
Professor Jay pamoja na marehemu Albert Mangwea ndiyo wasanii wake wawili bora
wa siku zote katika muziki wa Hip hop Tanzania.
“Wasanii
wangu bora kwa kipindi chote kwenye muziki wa Hip hop ni marehemu Albert
Mangwea pamoja na Professor Jay hiyo nasema na kuna siku nilishawahi kuandika
hilo, mpka Professor alinipigia simu na kuniuliza mzee una nini unataka kufa
nini?. Watu hawajui tu huyu Professor Jay kwanza ndiyo mtu aliyefanya muziki
wetu huu kwanza uanze kuheshimiwa, mwanzoni nyimbo zilikuwa na ujumbe wa fujo
fujo fulani, kwa hiyo muziki wetu ulikuwa hauchukuliwi ‘serious’ lakini baada
ya chemsha bongo kila kitu kikabadilika” alisema Mwana FA
Mbali na
hilo Mwana FA alisema kuwa Professor Jay ni msanii ambaye alifanya yeye kidogo
aache muziki sababu Mwana FA alikuwa anataka kufanya muziki bora lakini
alipokuwa anasikiliza kazi za Professor Jay akaona hawezi kufanya kazi bora
kama hizo.
“Unajua mimi
siku zote huwa nataka kuwa best kwa kile nachofanya sijui kwa wasanii wengine,
sasa baada ya kusikia ngoma ya Professor Jay ‘Chemsha bongo’ mimi nina nyimbo
zangu nilikuwa nimeandika nikarudi nyuma nakajiuliza sasa mimi nawezaje kuwa
‘best’ kwa ngoma hizi? Yaani alinikatisha tamaa lakini nikarudi na kuanza
kujipanga upya” alisema Mwana FA
No comments:
Post a Comment