
BAADA ya
kutolewa barua ya uchumba na mpenzi wake mpya, Chidi Mapenzi, mwigizaji, Shamsa
Ford, amefunguka kwamba wakati wowote atafunga ndoa na mwanaume huyo kwa kuwa
mipango yao imeshakamilika.
Shamsa
aliliambia MTANZANIA kwamba licha ya kupitia katika changamoto za wapenzi
wengi, mpenzi wake huyo wa sasa ndiye aliyeonyesha ushawishi hadi kutaka
kumuoa.
“Kwa hatua
hii najivunia, hadi mwanaume akushawishi muoane huyo ana nia njema na heshima
kwangu,” alisema Shamsa.
Pia Shamsa
aliwaeleza wapenzi wa filamu zake kwamba wataendelea kupata burudani zake hata
kipindi atakachokuwa ameolewa.
No comments:
Post a Comment