MSHAMBULIAJI Ibrahim Ajibu, juzi alifikisha mabao matano ya kufunga ndani ya mechi tatu za kirafiki za kujipima nguvu za timu yake ambayo imeweka kambi Chuo cha Biblia mjini Morogoro kujiandaa na msimu mpya.
Mshindi huyo wa tuzo ya Bao Bora la Msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, juzi aliifungia Simba mabao mawili wakati ikiilaza 5-0 dhidi ya Burkina Fasso ya Morogoro katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Highlands, Bigwa mkoani humo.
Mabao
mengine ya Simba inayofundishwa na Kocha Mcameroon, Joseph Omog, yalifungwa na
viungo Said Ndemla na wachezaji wapya, Mussa Ndusha kutoka DRC na Shiza Kichuya
kutoka Mtibwa Sugar.
Ajibu ambaye
mashabiki wake wanamuita ‘Cadabra’ wakimfananisha na mshambuliaji mpya wa
Manchester United, Zlatan Ibrahimovic, awali alifunga bao moja katika ushindi
wa 2-0 dhidi ya Moro Kids na mawili katika ushindi wa 6-0 dhidi ya Polisi
Morogoro.
Simba SC
itashuka tena dimbani Agosti 8, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
kumenyana na Interclube ya Angola katika mchezo wa kuazimisha miaka 80 ya klabu
hiyo, maarufu kama Simba Day
No comments:
Post a Comment