Suala la
Miundombinu kwa jiji la Dar es Salaam ni kitendawili ambacho kinazua majibu
mapya kila siku, baadhi ya barabara zimekuwa zikijengwa chini ya kiwango na
wakandarasi na kuzirudia barabara hizo, kwa upande wa halmshauri ya Ilala
kupitia baraza la madiwani wamepata mwarobaini wa suala hilo.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Mstahiki Meya Charles
Kuyeko ameeleza kuwa kufuatia malalamiko ya madiwani kuhusu suala la
miundombinu kwa maeneo ya Halmashauri hiyo, Mstahiki Meya ameeleza kuwa
wamehadiwa kupatiwa bilioni 93 na benki ya dunia endapo wataweza kulipa kiasi
cha shilingi milioni 8 zitakazo tumika kuwalipa wananchi ambao wamejenga maeneo
yaliyo katika hifadhi ya barabara.
Mstahiki
Meya Kuyeko ameendelea kufafanua kuwa tayari wameisha kopa kiasi hicho cha fedha hivyo wapo mbioni
kuanza zoezi hilo la ukarabati wa mindombinu ya barabara kwa kiwango
kinachostahili na mifereji ya maeneo mbalimbali, na Mkururugenzi wa Halmashauri
hiyo Msongela Nitu ameahaidi kushirikiana na baraza la madiwani kwa masuala
yote yenye tija kwa watanzania.
Huku kwa
upande wake Mbunge wa jimbo la Ukonga Bona Kaluwa akiiomba serikali kulitafutia
ufumbuzi suala la kupunguziwa vyanzo vya mapato kwa Halmashauri hiyo jambo
ambalo linawawia vigumu kama wajumbe wa baraza la madiwani kutekeleza baadhi ya
miradi ya maendeleo ukizingatia kuwa shughuli nyingi za serikali zinafanyika
Ilala kutokana na uwepo wa Ikulu.
No comments:
Post a Comment