Wanasema ni
ngumu kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu maarufu na kama utakubali kuwa
kwenye uhusiano huo basi inabidi uwe muelewa na mvumilivu maana utayoyasikia ni
mengi.
Mama Ivan
ambaye ni mke wa msanii wa hiphop Tanzania Roma Mkatoliki anasema amezoea kuona
headlines za mume wake magazetini lakini kuna moja ilimuumiza na hajaisahau
mpaka leo.
>> ‘Mimi sipendi skendo kuhusiana na mume wangu kikubwa na kusema ukweli ilitokea moja kwenye Magazeti kwamba Roma kuwa ana mtoto amezaa na Lotus iliniuma sana moyoni lakini mwisho wa siku nikabaini kwamba si kweli bali zilikuwa ni skendo‘
No comments:
Post a Comment