
Meneja wa
mwanamuziki wa kimataifa Diamond Platnumz, Hamis Tale Tale maarufu kwa jina la
‘Babu Tale’ hivi sasa yupo mikononi mwa polisi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam.
Babu Tale
amekamatwa leo na kufikishwa mahakamani hapo ili ajieleze ni kwa nini asifungwe
kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya Mahakama iliyomwamuru alipe fidia ya Sh250
milioni kwa makosa ya kuvunja sheria ya Hakimiliki.
Babu Tale
anatakiwa alipe fedha hizo kutokana na kuvunja mkataba kati yake na Shekhe
Mbonde, kwa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya shekhe
huyo, jambo ambalo ni kinyume na haki miliki.
No comments:
Post a Comment