
Mkali wa
wimbo ‘Kidogo’, Diamond Platnumz amethibitisha ujio wa mtoto wa pili kutoka kwa
mpenzi wake Zari.
Muimbaji
huyo amesema yeye na mpenzi wake Zari wanategemea mtoto wa kiume.
“Yah kweli
mimi ni baba kijacho,” Diamond alikiambia kipindi cha Leo Tena “Natarajia Mama
Tiffa anipatie tena mtoto mwingine, atakuwa wa kiume,”
Aliongeza,
“Na itakuwa mwezi Disemba mwaka huu! Baada ya hapo sitaongeza tena mtoto
mwingine, ni muda wa kula bata sasa ndio unafata na watoto wetu wawili”
Diamond na
Zari tayari wana mtoto mmoja wa kike, ‘Tiffa’ ambaye hivi karibuni atatimiza
mwaka mmoja.
No comments:
Post a Comment