Siku moja
baada ya mkutano mkuu wa Simba kufanyika na kukubali kupitisha maadhimio ya
mabadiliko ya kiuongozi ili klabu iendeshwe kwa mfumo wa hisa, bilionea wa 21
Afrika ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya Mohammed Enterprises
Tanzania Limited (MeTL) Mohammed Dewji ameelezwa kusikitisha na taarifa za
upotoshwaji.
Mohammed
Dewji amesikitishwa kutokana na taarifa zilizotolewa katika mkutano mkuu Simba
uliofanyika jana July 31 2016, kuwa yeye ambaye aliomba kununua asilimia 51 ya
hisa za Simba kama mfumo ukibadilishwa, hajaandika barua kwa uongozi wala
kukutana nao ila amekuwa akiongea kupitia vyombo vya habari kitu ambacho sio
kweli.
“Kiukweli
nimesikitishwa kwa wanaosema dhamira yangu ya kutaka hisa Simba nimeomba
kupitia vyombo vya habari na wala sijaandika barua, ukweli nimekutana na Rais
wa Simba Evans Aveva zaidi ya mara tatu, ameshakuja ofisi kwangu zaidi ya mara
tatu”
“Kuhusu
kuandika barua nilikuwa sijaandika kwa sababu mfumo wa hisa niliokuwa nahitaji
ulikuwa haupo sasa utaombaje kitu ambacho hakipo, ila leo baada ya mkutano mkuu
kukubali nimeandika barua rasmi kwenda kwa uongozi wa Simba na tayari
tumeshaituma”
Barua kutoka
Simba baada ya mkutano mkuu uliofanyika jana July 31 2016 kupitisha maadhimio
ya mabadiliko
No comments:
Post a Comment