Baada ya
mkutano mkuu wa klabu hiyo uliofanyika leo katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa
Polisi, Oyesterbay, ambao ulikuwa na ajenda 10, moja kati ya ajenda hizo
ilikuwa ikizungumzia taarifa ya kamati ya maboresho ya mfumo wa uendeshaji wa
klabu hiyo.
Katika
ajenda hiyo ndipo lilipojitokeza suala zima la MO ambapo wanachana hao wa Simba
zaidi ya 700 waliojitokeza kwenye mkutano huo walitaka bilionea huyo apewe timu
hiyo kutokana na hali mbaya ya kiuchumi iliyopo klabu hapo ambapo imekuwa
ikijiendesha kwa hasara kila mwaka.
Katika msimu
wa 2014/15 klabu hiyo ilifanikiwa kujikusanyia TSh bilioni 2, 096, 721, 493 kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali vya
mapato lakini ikatumia Sh bilioni 2,101,100,303 na kujikuta ikidaiwa 4,
378,810.
Lakini pia
katika bajeti yake ya msimu ujao wa 2016/17 uongozi huo unatarajia kukusanya
kiasi cha Sh bilioni 3, 583, 000,000 kutoka katika vyanzo vyake vya mapato
lakini matumizi yake yanatarajiwa kuwa Sh bilioni 4, 411,025, 000, hivyo
itakuwa ikidaiwa Sh milioni 828, 025, 000.
Kutokana na
hali hiyo wanacha hao waliutaka uongozi huo, kukubali kumpatia Mo timu kwani wanataka mabadiliko na wamechoshwa na
hali hiyo ya ukata wa kila wakati ambao umekuwa ukiwatesa na kuwakosesha amani
kila siku.
Hata hivyo
uongozi wa klabu hiyo chini ya rais wake, Evans Aveva haukuwa tayari kufanya
hivyo licha ya kelele za wanachama hao ambao kila wakati walikuwa wakiimba na
kulitaja jina la MO.
No comments:
Post a Comment