
TUZO mpya ya
video bora ya wimbo wa Bongo Fleva imekwenda kwa Farid Kubanda ‘Fid Q’ kupitia
video ya wimbo wake wa ‘Walk it Off’.
Katika
shindano hilo, wasanii saba wa muziki wa kizazi kipya kutoka Dar es Salaam na
watatu kutoka Uganda walioshindanishwa video zao, video hiyo ndiyo iliibuka
mshindi.
Kwa mujibu
wa mkurugenzi wa tamasha hilo, Profesa Martin Mhando, Fid Q atakuwa balozi wa
tamasha hilo kwa mwaka mzima na ataandaa wimbo wa tamasha hilo kwa mwaka ujao.
“Video hiyo
ndiyo iliyochaguliwa kuwa bora na majaji wetu, msanii wa video hiyo ndiyo balozi
wetu kwa mwaka mzima, naye ndiye atatunga na kurekodi wimbo wa Ziff kwa tamasha
lijalo,” alisema Profesa Mhando.
Baadhi ya
video zitakazoshindanishwa ni pamoja na ‘Aje’ wa Ali Kiba, ‘Sweet sweet’ wa
Chege Chigunda, ‘Zigo Remix’ wa Ay aliomshirikisha Diamond Platnumz na
‘Sizonje’ wa Mrisho Mpoto.
>>>HAYA NDIO MAKUBALIANO YA CLUB YA BAYERN NA DORTMUND, BONYEZA HAPA CHINI KUSOMA TAARIFA KAMILI!
No comments:
Post a Comment