
Mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Imara , Samwel Alcado (39) amekutwa akiwa amejinyonga ndani ya chumba chake kutokana na kile kinachodaiwa ni kugundulika kuwa ana virusi vya Ukimwi (VVU).
Mlinzi huyo
ambaye ni mkazi wa mtaa wa Mji wa Zamani Manispaa ya Mpanda amejinyonga kwa
kutumia shati lake.
Mwenyekiti
wa mtaa huo, Margret John amesema tukio hilo
limetokea leo majira
saa kumi na moja alfajiri ndani ya
chumba alichokuwa akiishi Alcado.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda amethibitisha kutokea kwa kifo hicho
akisema uchunguzi zaidi unaendelea kufanyika ili kubaini ukweli halisi wa tukio
hilo.
KAMA HUKUONA, BASI NIMEKUSOGEZEA TENA HIVI NDIVYO NGOMA ILIVYO HIT NAKUCHUKUA HEADLINES NYINGI, BONYEZA HAPA KUONA!
No comments:
Post a Comment