
BODI ya
wakurugenzi ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limewasimamisha kazi
wakurugenzi sita na meneja watano na Mhandisi mmoja kufuatia matumizi mabaya ya
ofisi na kutofuata sheria na kanuni.
Kwa mujibu
wa taafia iliyotolewa leo na Mkurugnezi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara imesema hatua ya
kuwasimamisha kazi wakurugenzi na mamenja hao inafuatia kikao cha bodi chini ya
uenyekiti wa Prefesa Samweli Wangwe
kilichokaa kuanzia Ijumaa iliyopita.
“Bodi
imeagiza kusimamishwa kazi Wakurugenzi ,
Mameneja watano na Mhandishi mmoja ili kupisha uchunguzi ili kubaini wahusika
katika tuhuma za ubadhirifu, matumizi mabaya ya ofisi na kutofuata kanuni,
sheria na utatibu katika uwekezaji,
usimamizi wa miradi na manunuzi ya ardhi na ajira,” alisema Profesa
Kahyarara.
CHEKI HII HUKO BARANI ULAYA, MAKUBALIANO YALIYOFANYIKA KATI YA TIMU YA BAYERN MUNICH NA DORTMUND, SOMA HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment