
Jeshi la
Polisi limekwama kuwafikisha mahakamani viongozi wanne wa Taifa wa Baraza la
Vijana la Chadema (Bavicha), baada ya kukosea hati ya mashtaka.
Wanaoshikiliwa
ni Mwenyekiti wa Taifa, Patrobas Katambi, Katibu Mkuu, Julius Mwita, Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji, Joseph Kasambala na Mwenyekiti wa Mkoa wa Mbeya, George
Tito.
Akizungumza
jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema makosa
yametokea wakati wa uandaaji wa hati ya mashtaka.
“Mahojiano yameisha, charge sheet (hati ya
mashtaka) ikaandaliwa, lakini ikarudishwa tuifanyie marekebisho. Muda umepita
wa Mahakama watapelekwa kesho (leo),” alisema.
Hata hivyo,
alisema kesi hiyo haina dhamana kwa upande wa kituo cha polisi na hivyo
kuwalazimu watuhumiwa hao kuendelea kukaa rumande.
“Wasubiri kesho (leo) wataka- poenda
mahakamani kama wataamua kuwapa dhamana,” alisema Mambosasa.
Kuhusu baadhi
ya watuhumiwa hao kugawanywa katika selo tofauti za Chamwino na wengine kuachwa
Kituo Kikuu cha Polisi, Mambosasa alisema huo ni utaratibu wa kawaida ambao
unalenga kupata maelezo ya kila mmoja.
“Hayo ni
mahojiano tu ili kila mmoja upate anasema nini ndipo unawaweka sehemu tofauti.
Hizo ni taratibu za mahojiano ili wasiendelee na mawasiliano,” alisema.
Makamu
Mwenyekiti wa Bavicha, Patrick Ole Sosopi alisema kisheria watuhumiwa
hawatakiwi kukaa rumande kwa zaidi ya saa 24.
“Cha
kusikitisha siku ya leo (jana) ambayo walisema wangewaleta mahakamani kwa kile
wanachoamini wametenda kosa, lakini hadi sasa muda wa mahakama unaisha viongozi
wetu hawajaletwa,”alisema na kuongeza:
“Na sisi
tunataka kuondoka ili tuone taratibu nyingine ambazo zinaweza
kutuhakikishia usalama wa viongozi wetu.
Hadi sasa viongozi wetu hawajaletwa mahakamani.”
Alisema hata
kama polisi wanawaona viongozi wao wanamakosa, kisheria hawawezi kukaa na mtu
kwa muda wa siku tatu bila kumfikisha mahakamani.
Alisema
utendaji wa polisi nchini ni tofauti na wa nje ya nchi ambapo kwa nchi za
wengine, polisi ni sehemu ya huduma na si ya mabavu.
Alisema hali hiyo inaleta kadhia na masumbuko
kwa Watanzania na hivyo kupunguza imani yao kwa jeshi hilo.
Wakili wa watuhumiwa hao, Fred Kalonga alisema
wamekuwa na wateja wao tangu siku walipokamatwa kwa kuhakikisha wanahojiwa kwa
mujibu wa sheria.
“Kwa mujibu wa ahadi za polisi kuwa leo (jana)
wanaletwa mahakamani. Kuanzia saa 1.30 asubuhi tuko mahakamani na sasa
inakwenda saa 9.30 alasiri hakuna mtuhumiwa aliyeletwa. Kimsingi muda wa
mahakama umeisha,” alisema.
Alisema yeye
na wakili mwenzake, Azack Mwaipopo walikuwa wanakwenda kufuatilia taratibu
nyingine za kisheria za kuwawezesha kupata dhamana.
“Tunakwenda
kufuatilia taratibu nyingine lakini sisi tupo tayari muda wowote wakiletwa
tutawadefend (tutawatetea) kwasababu tunaamini kwa mujibu wa maelezo ya wateja
wetu wapo sahihi kuliko tuhuma zinazowakabili,” alisema.
Wanachama wa
Chadema walikuwa katika viwanja vya mahakama tangu saa 2.00 asubuhi hadi saa
9.30 alasiri baada ya kuelezwa na wakili wa watuhumiwa kuwa viongozi wa Bavicha
hawatapelekwa mahakamani tena.
Viongozi hao
walikamatwa Ijumaa usiku katika baa ya Capetown walipokwenda kunywa na kula
chakula. Wanadaiwa kwa tuhuma za kukusudia kuikashfu Serikali.
Akizungumzia
mpango wa vijana wa Chadema kuzuia mkutano wa CCM utakaofanyika Julai 23 mjini
hapa, Sosopi alisema wanaiheshimu kauli ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman
Mbowe ya kuwataka kutokwenda kuzuia mkutano huo.
“Tunaiheshimu
kauli ya mwenyekiti na tunatambua kuwa vijana wengi nchi nzima wamejiandaa
kwenda kuzuia mkusanyiko huo, lakini sasa tunashughulika na hili la viongozi
wetu kukamatwa kwanza,”alisema.
Alisema
baada ya viongozi wao kupata dhamana wataitisha kikao cha Kamati ya Utendaji ya
Bavicha haraka ili kujadili suala hilo na watatoa msimamo kama wanakuja na
mkakati mwingine ama kuendelea na huohuo
No comments:
Post a Comment