
Baraza la
Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, limekifutia usajili wake wa kutoa huduma za
kitabu, Kituo cha Tiba Asilia cha ForePlan Kliniki kilichopo Ilala Bungoni
jijini Dar es salaam, kinachomilikiwa na Dkt. Juma Mwaka maarufu kama Dkt.
Mwaka, kwa madai kuwa kimekiuka taratibu za kitabu za tiba mbadala.
Hayo
yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dkt. Edmund Kayombo alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ukumbi wa Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Akizungumza
jijini Dar es salaam leo katika Mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa
Baraza hilo, Dk. Edmund Kayombo amesema kuwa kufutiwa kibali cha Dk. Mwaka
kunatokana na sababu nyingi ambazo amekuwa akikiuka licha ya kupewa maonyo na
barua juu ya utoaji huduma zake.
Amesema
sababu nyingine ni kuwa katika matangazo yake amesema anatoa tiba za kisasa
wakati hiyo elimu hana ya kufanya huo.
Wengine
waliofutiwa usajili ni Fadhaget Sanitarium kinachoendeshwa na Tabibu Fadhili
Kabujanja pamoja na Mandai Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Abdallah
Mandai
Hata hivyo
limetoa adhabu mbalimbali kwa kituo cha Aman Herbal Clinic kinachoendeshwa na
Tabibu Esbon Baroshigwa, na Tabibu Castory Ndulu wa Kituo cha Ndulu Herbal
Clinic wamepewa barua ya onyo.
Aidha
wengine wamesimashwa kwa miezi sita ambao ni Tabibu John Lupimo wa Lupimo
Suntarium Herbal Clinic pamoja na Tabibu Simon Rusigwa wa Sigwa Herbal Clinic.
No comments:
Post a Comment