
Mitandao ya
kijamii nchini Ethiopia imezimwa.
Waethiopia
waliamka Wikiendi wakajipata hawana huduma hizo za mitandao kama Facebook,
Twitter, Instagram na Viber.
Serikali
imefunga mitandao hiyo tangu Jumamosi usiku.
Msemaji wa
serikali ameiambia shirika la habari la AFP kuwa serikali ilichukua hatua hiyo
kama njia ya kuzuia wanafunzi wasivurugwe na ushawishiwa mitandao hiyo ya
kijamii.
Hatua hiyo
vilevile imetokea majuma kadhaa baada ya baadhi ya makaratasi ya mitihani
kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii na kulazimu serikali kufutilia mbali
mitihani hiyo iliyodukuliwa.
''Serikali
imechukua hatua hiyo kwa muda hadi siku ya Jumatano.
Tumegundua
kuwa mitandao ya kijamii huvuruga kabisa ratiba ya vijana na haswa wanafunzi'',
alisema msemaji wa serikali Getachew Reda .
Serikali
imechukua hatua hiyo kwa muda hadi siku ya Jumatano mitihani itakapokuwa
imekamilika
Hatu hiyo
bila shaka imewaudhi wanaharakati wa kupigania uhuru wa habari nchini Ethiopia.
Mwanabloggu
mashuhuri Daniel Berhane amechapisha kwenye mtandao wake wa Twitter maswali
ambayo anataka yajibiwe.
Je ni nani
aliyechukua uamuzi huu?
Aliwashauri
kina nani ?
kwanini
alichukua hatua hiyo?
Je hii
haitakuwa mwanzo wa tatizo lipya la kukandamiza uhuru wa kujieleza ?
No comments:
Post a Comment