
Leo July 23
2016 Mjini Dodoma unafanyika mkutano
mkuu maalum wa CCM ambao ajenda yake kubwa ni ya kumchagua Rais Dk. John
Magufuli kuwa mwenyekiti wa tano wa chama cha Mapinduzi ‘CCM’. Baada ya hotuba
ya Mwenyekiti wa chama hicho Jakaya Kikwete, katibu mkuu mstaafu Yusuph Makamba
alipata nafasi ya kuzungumza na kusema haya……
Ø 'Askofu Gwajima alisema uongo kwamba Jakaya
Kikwete hakutaka kumpisha Magufuli kuwa mwenyekiti' - Yusufu Makamba #MkutanoMkuuCCM
Ø 'Chama kinatoka mikononi mwa kada anayekataa
ufisadi kiasi cha kumtosa rafiki yake Lowassa'- Yusuph Makamba #MkutanoMkuuCCM
Ø 'Chama kinakwenda mikononi mwa muasisi wa
Mahakama ya mafisadi'-Yusuph Makamba #MkutanoMkuuCCM
Ø 'Wapinzani nataka mjue JK alikuwa anawabatiza
kwa maji huyu ajaye atawabatiza kwa moto'-Yusuph Makamba #MkutanoMkuuCCM
Ø 'Rais Magufuli hakukataa ushauri alikataa vimemo
kikiwemo cha kwangu, kuna mtu nilikuwa nampigia debe awe DC'-Yusuph Makamba
#MkutanoMkuuCCM
KAMA ULIPITWA NA TUKIO ZIMA , NIMEKUSOGEZEA MTU WANGU, BONYEZA HAPA CHINI!
KAMA ULIPITWA NA TUKIO ZIMA , NIMEKUSOGEZEA MTU WANGU, BONYEZA HAPA CHINI!
No comments:
Post a Comment