
“Boss
amemganda Dangote,ameisahau Tip Top” kutoka kwa Roma ni moja kati ya mistari
inayozungumziwa sana kwa sasa huku ikidaiwa kuwa Roma amemponda Babu Tale
ambaye ni mmoja wa mameneja wa Diamond na meneja wa Tip Top pia kwenye wimbo
wake wa kaa tayari.
Kwa upande
wake Roma amesema kuwa hakumaanisha kumponda meneja huyo kama watu wengi
wanavyodhani bali alitaka kufikisha ujumbe kuwa watu wasisahau walipotoka
lakini kwa njia ya kisanii zaidi.
“Tafsiri ya
mstari huo ni kwamba tusisahau tulipotoka,ningeweza tu kuandika hivyo lakini
kama msanii inabidi niwe mbunifu,ndio nikajenga hiyo picha na ndiyo maana watu
wameukumbuka zaidi” alifafanua Roma alipokuwa akihojiwa na HZB TV
ANGALIA GARI
MPYA YA KIFAHARI ILIYOTENGENEZWA KWA TEKNOLOJIA YA JUU ZAIDI, BONYEZA HAPA
CHINI KUONA:
No comments:
Post a Comment