
Amini
usiamini Rais Yoweri Museveni, alishuka kutoka kwenye gari lake rasmi akachukua
kiti chake na kukiweka kando kando ya barabara mpya ya Isingiro ikipitia kijiji
hicho cha Kyeirumba hadi Tanzania na kupokea simu faraghani.
Mzee
Museveni kama vile baba wa taifa alitumia muda wake kufanya shughuli hiyo huku
akiwapungia mkono wapita njia.
Baada ya
dakika 30 hivi raia wa kijiji hicho walishangaa kuwa miongoni mwa maafisa wakuu
serikalini.

Ilikuwa
ajabu sana kwao kumuona Museveni akiwa ameketi barabarani.
Museveni
ampandisha cheo mwanaye jeshini
Waganda
katika mitandao ya kijamii wamesambaza picha hiyo ya rais museveni akizungumza
kwa simu ambayo inaonekana kuwa sio ya kisasa.
Je wewe
umewahi kuchukua hatua gani ya kushangaza ili upokee simu ya kibinafsi?
Wengine
wanamkejeli kwa kuhofia kudukuliwa huku wengine wakimkosoaa kwa kuketi
barabarani.
''Kwani
hangeweza kupokea simu yake ndani ya gari lake?"
''Ni siri
gani hiyo ambayo hakutaka hata walinzi wake wasikie.
''Ama
ilikuwa ni #Besigyexit?", wakizungumzia kuachiliwa kwa dhamana kwa
kiongozi wa upinzani Dkt Kizza Besigye mapema asubuhi.
No comments:
Post a Comment