Mshambuliaji
wa zamani wa Arsenal Thierry Henry ambaye amestaafu soka na kuingia kwenye kazi
ya ukocha katika klabu yake ya zamani ya Arsenal, Juy 12 2016 ameamua kutangaza
maamuzi magumu kuhusu ajira yake ndani ya klabu ya Arsenal.
Henry
ameamua kuacha kazi ya kuendelea kukifundisha kikosi cha vijana cha Arsenal,
baada ya kocha mkuu wa Arsenal Arsene Wenger kuamua kumwambia kuwa achague moja
kama kufanya kazi ya ukocha ndani ya Arsenal au kuendelea na kazi ya uchambuzi
wa soka katika kituo cha Sky Sports.
Baada ya
kauli ya Wenger imemfanya Thierry Henry ameamua kuacha kazi Arsenal na
kuendelea na kazi yake ya uchambuzi, kama utakuwa unakumbuka vizuri Henry
aliwahi kuichezea Arsenal katika kipindi cha miaka zaidi ya 7 na baadae kwenda
kucheza soka katika klabu ya New York Red Bulls ya Marekani.
No comments:
Post a Comment