
Mtoto wa
kike, Rahila Salim Ali (4) amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa
umening’inizwa kisimani na vidole vya mikono vikiwa vimekatwa na mashavu
kuchubuliwa.
Tukio hilo
limetokea jana asubuhi, katika eneo Njiapanda, Mbagala, Temeke baada ya mtoto
huyo kutoweka nyumbani siku nne zilizopita.
Akizungumzia
tukio hilo, mama mzazi wa mtoto huyo, Raziah Ramadhani alisema binti yake
alitoweka nyumbani saa tano asubuhi, wakati wakiwa pamoja wakitazama
televisheni.
“Alitoka nje
kama anaenda kucheza na wote hatukuwa na wasiwasi. Baada ya saa moja tulishtuka
baada ya kutomuona, hivyo ikabidi tuanze kumtafuta,” alisema.
Alisema
walitoa taarifa polisi na kwenye baadhi ya vyombo vya habari bila mafanikio
hadi jana mwili wake ulipokutwa umening’inizwa kwenye kisima cha nyumba ya
jirani yao.
“Nilipofika nilishangaa kuona nguo zake ni
kavu na ana majeraha,” alisema.
ANGALIA AJALI MBAYA YA BASI =>BONYEZA HAPA
Alisema
kisima hicho kina tundu dogo ambalo huenda wauaji walijitahidi kuusukumiza
mwili huo ili ionekane kama amefia humo ikashindikana.
Alisema
mpaka juzi mchana, kilikuwa kikitumika na kuwa huenda mwili huo ulining’inizwa
usiku wa kuamkia jana.
Baadhi ya
majirani waliliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina na kuwachukulia
hatua watu ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
Kamanda wa Polisi Temeke, Andrew Satta alisema
wanaendelea na uchunguzi: “Taarifa zilizopo ni kwamba amekufa maji lakini kwa
hayo mazingira mengine tunaendelea kufanya uchunguzi zaidi.”
AJALI MBAYA YA BASI LA NGORIKA =>BONYEZA HAPA
No comments:
Post a Comment