
KATIKA
harakati za kuhakikisha wafuasi wa vyama vya upinzani nchini zinazimwa, Jeshi
la Polisi mkoani Dodoama limewatia mbaroni viongozi wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), anaandika Dany Tibason.
Waliokamatwa
na jeshi hilo ni viongozi wa kitaifa wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha)
wakiwa wanakula na kunywa katika Bar ya Cape Town mjini humo.
Hata hivyo
zoezi la kuwakamata viongozi hao linaendelea hata pale ambapo mtu yoyote
anayeonekana kuwa, amevaa fulana zenye maneno yenye kaulimbiu za Chadema.
Tukio hilo
limekuja ikiwa ni siku chache tangu jeshi hilo, kuzuia mahafali ya Umoja wa
Wanavyuo Chadema (CHASO) kwa kuamuru wahusika waliokuwa wamekusanyika kwenye
Hoteli ya African Dreems, mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick
Sumaye kutawanyika.
Askari wenye
mabomu ya machozi, silaha za moto na gari moja la maji ya kuwasha, walizunguka
eneo la hoteli hiyo huku kiongozi wa polisi akitangaza;
“Ilani,
ilani, imeamriwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, wote mliokusanyika mahali
hapo mtawanyike, vinginevyo nguvu itatumika.”
Mahafali
hayo hayakufanyika kwa wanavyuo na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya
upinzani, kuondoka eneo hilo huku serikali mkoani humo ikieleza kuwa chanzo ni
taarifa za uwepo wa ugonjwa wa ajabu, uliyodaiwa kuibuka wilayani Chemba na
Kondoa.
Hata hivyo,
siku chache baadaye, Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli, alitangaza zuio la
kufanyika mikutano ya kisiasa ya hadhara na ya ndani pamoja na maandamano
akisema wakati wa uchaguzi umepita shughuli za kisiasa zipumzishwe mpaka
kipindi cha uchaguzi ujao, ili watu wafanye kazi za maendeleo.
Akizingumza
kwa njia ya simu leo Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma,
amethibitisha viongozi wa Bavicha kukamatwa wakituhumiwa kukusudia kuhamasisha
kuikashifu serikali.
Amesema,
hawatadhaminiwa mpaka Jumatatu, watakapofikishwa mahakamani.
Joseph
Kasambala, Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema-Taifa ametaja waliokamatwa kuwa ni
Patrobas Katambi, Mwenyekiti wa Bavicha- Taifa, Julius Mwita, Katibu wa Bavicha
-Taifa na George Tito, Mwenyekiti wa Bavicha mkoani Mbeya.
Akielezea
ilivyotokea, Kasambala amesema, walikuwa katika ziara kwenye baadhi ya mikoa,
walianzia mkoani Mara, katika Kijiji cha Mwitongo, Mwanza kabla hawajafika
Dodoma juzi Saa 8:00 mchana.
Amesema leo walikusudia
kukutana na vyombo vya habari mjini Dodoma, kuelezea hatua iliyofikiwa katika
mpango wao wa Bavicha – Taifa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Dodoma,
kuzuia wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanya mkutano mkuu wa taifa, 23
mwezi huu.
Amesema,
wakiwa Cape Town, majira ya usiku aliwaacha wenzake na kwenda kukutana na jamaa
yake mwingine na kwamba baadaye alipata taarifa za wenzake kukamatwa na polisi.
Amesema
kilichomsikitisha ni kukataliwa kuonana nao, alipofika kwenye kituo cha polisi
cha kati jana asubuhi ambapo alitakiwa kwanza akaonane na viongozi wa polisi wa
wilaya na mkoa (OCD, RPC).
Pia ameeleza
kwamba, taarifa alizopatiwa kwenye kituo hicho cha polisi zimeeleza kuwa kosa
wanalotuhumiwa kufanya ni kuikashifu serikali, kwa kuvaa T/shirt yenye
maandishi “Dikteta Uchwara”.
Hata hivyo,
Kasambara amesema, madai hayo ni ya uongo huku akionesha maandiko yaliyo kwenye
fulana aliyokuwa amevaa, yenye rangi nyeusi na maandiko meupe yanayosema;
“Mwl.
Nyerere; Demokrasia inanyongwa” upande wa mbele huku upande wa nyuma ikisomeka;
“Haki na Amani.
Amesema,
ziara yao inajumuisha viongozi sita wa Bavicha, akiwataja kuwa pamoja na yeye,
watatu waliokamatwa ni Edward Simbeye, Katibu Mwenezi wa Bavicha–Taifa na
Katibu wa Bavicha – mkoani Temeke, Hilda
No comments:
Post a Comment