
Habari ya
mjini! Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe, anadaiwa kunasa
ujauzito wa mwandani wake ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Rajab Abdulhan
‘Harmonize’ hivyo yupo mbioni kutimiza ndoto yake ya kupata mtoto hivi
karibuni.
Habari za
uhakika kutoka kwa watu wa karibu wa mastaa hao zilidai kwamba, ishu hiyo ni
mpango wa wasanii hao kwa kuwa walipanga mwanzoni wakati wa kuanzisha uhusiano
wao hivyo kwa tukio hilo kila mmoja ana furaha na wamejipanga kumpokea mgeni
wao.
Chanzo hicho
kilimwaga ubuyu kwamba, hivi karibuni, Wolper na Harmonize waliingia kwenye
mgogoro kidogo lakini lilipoibuka suala la mrembo huyo kunasa ujauzito, ndipo
uhai wa penzi lao ukarejea kwa kiwango cha juu.
“Ni kweli
hapo nyuma walizinguana lakini baada ya mimba, sasa hivi penzi lao lipo kwenye
ubora wake na kila mmoja anafurahia jambo hilo kwa sababu wamejipanga,”
kilisema chanzo hicho.
Baada ya
kunyetishiwa ishu hiyo, Wikienda lilimsaka Wolper ili kuthibitisha madai hayo
ambapo alisema kuwa kama tulivyoipata habari hiyo, kama ni kweli hakuna tatizo
lolote yeye kupata ujauzito.
“Jamani
habari nyingine ni njema sana, kama kuna mtu amewaambia basi siyo mbaya maana
nipo huru kuwa mjamzito kwani sijasababisha chochote kibaya kwa mtu,” alisema
Wolper huku Harmonize akisisitiza kuwa Wolper ndiye msemaji pekee wa suala
hilo.
DIAMOND NA WEMA MAMBO YAZIDI KUNOGA =>ONA HAPA
CHANZO Udaku special
No comments:
Post a Comment