
Katika
kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ombaomba 60
wamekamatwa katika msako unaoendelea.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Grace
Magembe amesema wamewakamata 60 na operesheni inaendelea.
“Ukamataji
wa ombaomba katika jiji la Dar es Salaam unaendelea, 60 wamekamatwa na
kufunguliwa mashtaka,” amesema Dk
Magembe.
Amesema
miongoni mwa ombaomba hao, wapo watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 ambao wamepelekwa katika vituo vya watoto
yatima, kikiwamo Kituo cha Kurasini.
Dk Magembe
amesema bado ombaomba wamekuwa
wakionekana jijini Dar es Salaam
kutokana na kuwapo kwa watu wanaotoka mikoani na kuingia katika makundi ya
ombaomba kila siku.
Amesema uongozi wa mkoa unashirikiana na Wizara ya
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kutoa elimu mikoani kuhusu
operesheni ya kuwaondoa ombaomba.
Amesema
ombaomba wengi wanakuja kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.
Awali Makonda alitangaza operesheni kubwa ya
kuondoa ombaomba katika Jiji la Dar es Salaam.
aliwataka
polisi kwa kushirikiana na ustawi wa jamii kuwaondoa ombaomba wote waliopo
mitaani.
Pia, Makonda
amepiga marufuku wananchi wanaowapa fedha ombaomba kuacha mara moja ili wajitafutie riziki
wenyewe kwa kufanya biashara au kurudi mikoani kujishughulisha na kilimo.
KAMA HUKUONA LILE SHAMBULIO LA KIGAIDI KULE UFARANSA , BONYEZA HAPA CHINI KUONA TUKIO ZIMA!!
No comments:
Post a Comment